Home Biashara Wakulima wa maziwa kupata mapato zaidi, asema Gachagua

Wakulima wa maziwa kupata mapato zaidi, asema Gachagua

0

Wakulima wa maziwa wanatazamiwa kupata mapato zaidi kufuatia hatua ya serikali kuingilia kati suala la kuwepo kwa maziwa mengi ambako kumetishia kuathiri bei za juu za maziwa.

Naibu Rais Rigathi Gachagua anasema serikali imeingilia kati kwa kuitengea kampuni ya Kenya Cooperative Creameries, KICC shilingi milioni 900 ili kununua maziwa na hivyo kuepusha bei za maziwa kupungua kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji.

Kwa sababu ya serikali kuingilia kati, bei za maziwa zitapanda hadi shilingi 50 kwa lita kutoka shilingi 45 kuanzia Machi 1, 2024. Naibu Rais alisema wanapania kuongeza bei hizo hadi zaidi ya shilingi 60 kwa lita miezi inayokuja.

“Kama serikali, tulitoa shilingi milioni 900 ili kudhibiti bei katika sekta ya maziwa kufuatia ongezeko la maziwa lililotokana na mvua kubwa. Bei katika KICC zitaongezwa kutoka shilingi 45 kwa lita hadi shilingi 50 kwa lita kuanzia Machi mosi na hadi shilingi 60 katika miezi ijayo,” aliahidi Gachagua.

Naibu Rais aliwataka wakulima wa maziwa kuiuzia kampuni ya KCC maziwa yao ili kupata mapato zaidi.

Aliyasema hayo akiwa katika eneo bunge la Kwanza, kaunti ya Trans Nzoia ambako pia aliongoza hafla ya uchangishaji fedha.

Martin Mwanje & DPCS
+ posts