Home Biashara Wakulima wa Majani chai kunufaika na mapato yaliyoimarika

Wakulima wa Majani chai kunufaika na mapato yaliyoimarika

Chini ya mpango huo mpya, kampuni hizo mbili zitatangaza  majani chai ya Kenya kuwa ya ubora wa hali ya juu katika soko la kimataifa.

0
Rais William Ruto akutana na wawakilishi wa Liptons Teas na ile ya Infusions and Brown Investments.
kiico

Wakulima wa majani chai hapa nchini wanasababu ya kutabasamu, kwa kuwa mapato yao yataimarika kufuatia mkataba kati ya Kenya na kampuni ya Liptons Teas na ile ya Infusions and Brown Investments.

Chini ya mpango huo mpya, kampuni hizo mbili zitatangaza  majani chai ya Kenya kuwa ya ubora wa hali ya juu katika soko la kimataifa.

Ushirikiano huo, utashuhudia kampuni hizo zikishirikiana na wakulima wa hapa nchini kuboresha uwezo wa sekta ya majani chai.

Mpango huo unajumuisha kuanzishwa kwa hazina ya uwekezaji, huku shilingi bilioni moja zikiwekwa kwa hazina hiyo kufadhili miradi ya kijamii.

Tayari kampuni ya Liptons iko katika harakati za kuanzisha taasisi ya Lipton’s Tea, ambayo itatoa mafunzo kwa wakulima kuhusu mbinu bora zitakazowezesha kupata mazao ya ubora wa hali ya juu.

Kampuni hizo pia zitajenga kiwanda cha kisasa cha kuzalisha mbolea ya majani chai.

Rais William Ruto, alisema majani chai ya Kenya itavutia soko la kimataifa kutokana na ubora wake wa hali ya juu.

Rais aliyasema hayo leo Jumanne alipokutana na wawakilishi wa kampuni hizo mbili katika Ikulu ya Nairobi.

Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na balozi wa Sri Lanka hapa nchini Veluppillai Kananathan, miongoni mwa wengine.

kiico