Home Kaunti Wakulima huko Imenti wahimizwa kujisajili

Wakulima huko Imenti wahimizwa kujisajili

Mbunge wa eneo la Imenti ya kati Moses Kirima amesihi wakulima wa eneo lake wajisajili kwenye mpango wa usambazaji wa mbolea ya bei nafuu kama mojawapo ya mipango ya serikali kuu ya kukabiliana na ukosefu wa chakula cha kutosha nchini.

Akizungumza katika eneo bunge lake, kiongozi huyo alisihi wakulima wajibidiishe kwenye mashamba yao, hasa msimu unaokuja wa upanzi, kwani kilimo ndiyo njia pekee ya kuhakikisha uwepo wa chakula cha kutosha nchini na hatimaye kupunguza gharama ya maisha.

Mheshimiwa Kirima alifafanua kwamba wakulima wa eneo hilo watapata mbolea hiyo ya bei nafuu kwenye kiwanda cha kahawa kilicho karibu, kinyume na awali ambapo walikuwa wanakwenda hadi mjini Meru kupata mbolea kutoka kwenye ghala la bodi ya nafaka na mazao NCPB.

Alisisitiza umuhimu wa wakulima kutekeleza jukumu lao la kujisajili bila kuzingatia ukubwa wa ardhi yao ya kilimo akisema serikali kuu chini ya uongozi wa Rais William Ruto iko ange kusaidia wakulima kwa kuhakikisha pembejeo za kilimo zinapatikana kwa bei nafuu ili wazalishe chakula zaidi.

Website | + posts
Marion Bosire & Jeff Mwangi
+ posts
Jeff Mwangi
+ posts