Home Kimataifa Wakfu wa KEPSA, Mama Doing Good zaingia kwenye mapatano

Wakfu wa KEPSA, Mama Doing Good zaingia kwenye mapatano

0

Wakfu wa muungano wa sekta ya kibinafsi nchini – KEPSA Foundation – umetia saini mkataba na shirika la mkewe rais la Mama Doing Good, kwa lengo la kuunda kwa pamoja mapendekezo ya kutafuta ufadhili wa mipango yao.

Mkataba huo pia unalenga kutekeleza mipango ambayo itahimiza utangamano wa kitaifa na uadilifu, utunzi wa mazingira na tabianchi, kuwapa wanawake uwezo pasi kusahau maadili ya familia.

Mashirika hayo mawili yatafanya utafiti wa kuona uwezekano wa kutoa huduma kama kuandika mapendekezo ya kitafuta ufadhili wa mipango waliyokubaliana kama kutunza mazingira, kudhibiti tabianchi na kuwezesha wanawake kiuchumi.

Watatafiti pia uwezekano wa kubadili sera katika nyanja lengwa ili kuhakikisha uhamasisho kupitia kwa mafunzo na kushirikiana katika utoaji mafunzo kwa sekta ya kibinafsi kuhusu jinsi ya kuanzisha biashara endelevu.

Kando na hayo, KEPSA na Mama Doing Good watachunguza iwapo wataboresha ushirikiano kati ya kampuni kubwa na ndogo hasa za makundi yaliyotengwa pamoja na kutoa usaidizi wa kiufundi kwa biashara mbali mbali katika kuunganisha maswala ya kutunza mazingira, kudhibiti tabianchi na kuinua wanawake kwenye mipangilio ya biashara zao.

Akizungumza wakati wa kutia saini mkataba huo kwenye afisi ya mkewe rais, mkurugenzi mtendaji wa wakfu wa KEPSA Gloria Ndekei alidhihirisha imani kwamba watafanikiwa kutekeleza mambo ambayo yako kwenye mkataba huo.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa shirika la Mama Doing Good Dr. John K. Chumo alishukuru wakfu wa KEPSA kwa kukubali kushirikiana nao akisema safari ya ushirikiano huo ilianza mwisho wa mwaka 2022 na wamefanikisha kazi nyingi pamoja hata kabla ya kuingia kwenye mapatano.

Website | + posts