Home Habari Kuu Wakenya watakiwa kutahadhari msimu wa shamrashamra

Wakenya watakiwa kutahadhari msimu wa shamrashamra

0

Katibu katika Wizara ya Usalama wa Taifa Dkt. Raymond Omollo amewataka Wakenya kuchukua tahadhari msimu wa sherehe za Krimasi na Mwaka Mpya.

Omollo alisema haya jana Jumapili alipohudhuria ibada katika kanisa la St. Barnabas Catholic eneo la Matasia, kaunti ya Kajiado.

Katibu huyo aliahidi kuwa serikali itaongeza magari ya polisi na kuimarisha hali ya vituo vya polisi katika eneo hilo.

Omollo amefichua kuwa serikali itabuni kata mpya zaidi katika kaunti ya Kajiado ili kusongeza huduma za serikali karibu na wananchi.

Website | + posts