Home Kimataifa Wakenya wapongezwa kwa kushiriki upanzi wa miti

Wakenya wapongezwa kwa kushiriki upanzi wa miti

Waziri Tuya aliwahimiza wakenya kusendelea kupanda miti wakati huu wa msimu wa mvua, kipindi ambacho serikali inalenga kupanda miti milioni 500, kabla ya msimu wa krismasi.

0
kra

Waziri wa mazingira, mabadiliko ya tabia nchi na misitu Soipan Tuya, amewapongeza wakenya kwa kuitikia wito wa upanzi wa miti, katika juhudi za serikali za kupanda miti bilioni 15 kufikia mwaka 2032.

Kupitia kwa taarifa siku ya Jumanne, Tuya alisema wakenya walionyesha uzalendo wa hali ya juu wakati wa siku ya kitaifa ya upanzi wa miti siku ya Jumatatu, ambapo serikali iliafikia lengo la kupanda miti milioni 150.

kra

“Habari tunazopokea kutoka pembe zote za nchi, zinaashiria kwamba tumeafikia lengo la kupanda miti milioni 150, huku mtandao wa ‘Jaza Miti’, ukiashiria usajili 7,000 mpya. Tunawasihi wale waliopanda miti jana lakini haikunakiliwa, kufanya hivyo kupitia mtandao huo,” alisema Waziri Tuya.

Aidha Waziri huyo aliwahimiza wakenya kusendelea kupanda miti wakati huu wa msimu wa mvua, kipindi ambacho serikali inalenga kupanda miti milioni 500, kabla ya msimu wa krismasi.

Serikali inalenga kutumia mtandao wa ‘Jaza Miti’, kufuatilia zoezi la upanzi wa miti, huku watumiaji wa mtandao huo wakiwa na fursa ya kuchagua aina za miti wanayoweza kupanda katika maeneo yao.