Maelfu ya Wakenya wamemiminika mapema Ijumaa katika uwanja wa Kericho Green kwa maadhimisho ya sherehe za 60 za siku kuu ya Mashujaa.
Sherehe za mwaka huu zinaadhimishwa chini ya kauli ya kueneza afya ya nyumbani maarufu kama community health promoters, kupitia kwa mpango wa serikali wa afya kwa wote maarufu kama UHC.
Serikali imewaajiri wahudumu laki moja wa kutoa afya ya nyumbani shilingi mpango wote wa utoaji afya kwa wote ukigharimu shilingi blioni 500 .
Rais William Rutio alisaini miswaada minne ya huduma za afya siku ya Alhamisi ikiwemo ile ya Primary Health Care Bill, the Facility Improvement Financing Bill, the Digital Health Bill na the new Social Health Insurance Bill.