Home Kimataifa Wakenya wahimizwa kuunga mkono mabadiliko katika Baraza la Mawaziri

Wakenya wahimizwa kuunga mkono mabadiliko katika Baraza la Mawaziri

Naibu huyo wa Rais alilaani uharibifu wa mali na ghasia wakati wa maandamano ya amani yaliyoandaliwa na vijana wa Gen Z.

0
Naibu Rais Rigathi Gachagua.
kra

Naibu Rais Rigathi Gachagua, amewahimiza wakenya kudumisha umoja na kuunga mkono mabadiliko yaliyofanywa na Rais William Ruto katika Baraza la Mawaziri.

Kulingana na Gachagua, mabadiliko hayo katika Baraza la Mawaziri yatachochea kuafikiwa kwa ufanisi nchini, huku akiwakashifu wanaojaribu kuwagawanya wakenya.

kra

“Watu wengine wanachanganua kuhusu nani alishinda au kushinwa, lakini swala hilo nzima ni ushindi kwa watu wote wa Kenya,” alisema Gachagua.

Gachagua aliyasema hayo jana Ijumaa katika kijiji cha Ntukuruma, Nanyuki kaunti ya Laikipia wakati wa mazishi ya Susan Muthoni Kiiru Wanjohi (80), ambaye ni mamake katibu wa Baraza la Mawaziri.

Naibu huyo wa Rais alilaani uharibifu wa mali na ghasia wakati wa maandamano ya amani yaliyoandaliwa na vijana wa Gen Z.

“Tuendelee kudumisha umoja. Tumepitia kipindi kigumu. Wale ambao walichukua fursa ya maandamano ya amani kupora mali na kuwajeruhi wengine ni wapumbavu,” aliongeza naibu wa Rais.

Wakati huo huo Gachagua, aliwakashifu wale ambao walitumia fursa hiyo kueneza Propaganda, akidokeza kuwa wakenya ni watu werevu.

Aidha aliwahimiza walioteuliwa katika Baraza Jipya la Mawaziri kuwahudumia wakenya kwa bidii na kuwaheshimu raia wa Kenya, punde tu watakapoidhinishwa na bunge la taifa.