Home Kimataifa Wakenya wahimizwa kutahadhari kuhusu magonjwa yanayoathiri wanyama na binadamu

Wakenya wahimizwa kutahadhari kuhusu magonjwa yanayoathiri wanyama na binadamu

kra

Wananchi wamehimizwa kuwa waangalifu wanapotunza mifugo, kutangamana na wanyama wa porini na kutumia bidhaa zinazotokana na mifugo hasa wakati huu wa mvua ili kuepuka magonjwa yanayoathiri wanyama na binadamu kama “Rift Valley Fever”.

Uwezekano wa kuzuka kwa ugonjwa huo upo ikizingatiwa hali ya sasa ya anga.

kra

Wakizungumza huko Maralal, kaunti ya Samburu wakati wa kikao ambapo kamati maalum ilibuniwa kuongoza mkakati wa “One-Health” unaoangazia afya ya binadamu, mifugo na wanyama sawia na ule wa kaunti ya Isiolo, wadau wa sekta ya afya ya umma na madaktari wa mifugo walisema hali ya sasa ya anga inapendelea magonjwa kama hayo.

Kwa sababu hiyo wanahimiza uangalifu watu wanapotumia bidhaa za mifugo kama vile maziwa na nyama.

Pius Kerio, wa idara ya utafiti wa magonjwa katika kaunti ya Samburu alishauri wakenya kuhakikisha kwamba nyama ambayo wanakula imekaguliwa na tabibu wa mifugo na imepikwa vizuri.

Aliongeza kusema kwamba magonjwa yanayoambukizwa binadamu na mifugo kama kimeta na homa ya bonde la ufa yanaweza kusababisha maafa kwa binadamu.

Mkakati wa “One Heath Approach” unazinduliwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya kaunti ya Samburu, shirika la VSF Suisse na lile la Biovision.

Kamati tekelezi inajumuisha maafisa kutoka idara za afya ya umma, matabibu wa mifugo na huduma ya wanyamapori KWS kati ya wengine.

Website | + posts
Bruno Mutunga
+ posts