Home Habari Kuu Wakenya wahimizwa kufanya vipimo vya kiafya kila mara

Wakenya wahimizwa kufanya vipimo vya kiafya kila mara

0

Mbunge wa Kipipiri Wanjiku Muhia amehumiza wakenya wawe wakifanyiwa vipimo vya kiafya kila mara ili kubaini magonjwa mapema na kutibiwa.

Akizungumza katika shule ya msingi ya Rironi huko Wanjohi katika mpango wa matibau bila malipo, mbunge huyo alisema kwamba magonjwa mengi ambayo hugharimu pesa nyingi kutibu, yanaweza kutibiwa kwa pesa kidogo iwapo yatabainishwa mapema.

Mpango huo wa matibabu bila malipo uliandaliwa na afisi ya mbunge huyo kwa udhirikiano na Lions international.

Alisema kisukari ni ugonjwa ambao umeathiri watu wengi sana katika eneo bunge lake la Kipipiri na kaunti nzima ya Nyandarua kutokana na lishe duni na uzee.

Wanjiku hata hivyo, alisema kwamba mabadiliko yaliyopendekezwa katika bima ya matibabu nchini NHIF yakitekelezwa, kila mkenya, hata wa mapato ya chini, ataweza kupata matibabu.

Mbunge huyo alihimiza wasomi wanaonfanya kazi mbali na nyumbani, wajizoehshe kusaidia jamii kwani hatua hiyo itamotisha walio shuleni kuiga mfano wao.

Watu zaidi ya elfu moja walifanyiwa vipimo mbali mbali wakati wa mpango huo huku waliobainika kwamba wanahitaji upasuaji wakiahidiwa kufanyiwa

Website | + posts