Home Burudani Wakenya waadhimisha siku ya wapendanao

Wakenya waadhimisha siku ya wapendanao

0

Wakenya leo Jumatano, wameungana na dunia nzima kusherehekea siku ya wapendanao, Valentine, kama ishara ya upendo kwa jamaa, marafiki na wapenzi wao.

Jijini Nairobi, maduka yalipambwa kwa bidhaa nyekundu kuvutia wateja, huku shuguli kochokocho za uuzaji na ununuzi wa maua, mavazi na bidhaa zingine nyekundu zikinoga.

Kwenye sehemu za kazi, baadhi ya wafanyakazi walivalia mavazi mekundu na hata wengine kubeba maua kuwapelekea wafanyakazi wenza.

Sehemu za kupiga picha hazikuachwa nyuma, zilifurika watu hasaa wapenzi wanaosherekea upendo wao kwa kupiga picha kama ishara ya kumbukumbu ya siku hiyo.

Sehemu za burudani nazo zimeonekana kupambwa vyema kwa ajili ya wateja wengi hasa familia na wapenzi wanaotarajiwa kufurika humo baada ya kazi.

Lakini je, siku ya wapendanao ilianza vipi?

Katika karne ya tatu baada ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, Askofu Valentine kutoka Italia aliuawa na utawala wa Kirumi kwa ajili ya kuendeleza ukristo nchini humo na ndipo jina lake likaenziwa hadi sasa kutokana na upendo wake kwa watu wote hata alipokuwa gerezani.

Boniface Musotsi
+ posts