Home Taifa Matumizi ya pombe na mihadarati: Wakenya milioni 4 wahitaji usaidizi

Matumizi ya pombe na mihadarati: Wakenya milioni 4 wahitaji usaidizi

0
kra

Wakenya wapatao milioni 4 wanahitaji huduma za ushauri nasaha na urekebishaji mienendo. Haya ni kulingana na taarifa ya katibu wa usalama wa taifa Raymond Omollo.

Katika taarifa hiyo iliyosomwa kwa na Bi. Beverly Opwora wakati wa uzinduzi wa mpango wa kimkakati wa shirika la kupambana na matumizi ya pombe na mihadarati nchini NACADA wa mwaka 2023-2027, Omollo alifafanua kwamba pombe na bhangi ndivyo vinatumiwa sana na wanaotumia kwa wingi ni vijana walio katika taasisi za elimu.

kra

Alisema pia kwamba nusu ya vijana hao sasa wamekuwa waraibu wa pombe na bhangi.

Mpango huo wa kimkakati unaangazia juhudi mpya za kukabiliana na changamoto zilizopo kama vile kuingizwa kwa mihadarati nchini kimagendo, bidhaa gushi, mauzo ya bidhaa ambazo hazijasajiliwa, kukosa kulipa ushuru na pombe haramu.

Omollo alisema kwamba matumizi ya pombe na mihadarati ni tishio la kitaifa kwa usalama wa wananchi na husababisha vifo watu wanapotumia pombe mbaya, watu kushindwa kufanya kazi, kupata matatizo ya kiafya na kuongezeka kwa visa vya uhalifu.

Tabia ya madereva kuendesha magari wakiwa walevi pia ni kisibabishi kikubwa cha ajali ambazo husababisha vifo na majeraha mabaya.

Mwaka huu pekee lita milioni 2.8 za pombe gushi na haramu zimenaswa pamoja na kilo elfu 6 za bhangi na washukiwa wapatao elfu 30 wamekamatwa kote nchini.

Maeneo ya nchi yaliyoathirika zaidi na pombe na mihadarati ni Nairobi, eneo la kati, eneo la bonde la ufa, Nyanza na magharibi mwa nchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here