Wakenya Mary Ngungi-Cooper na Abel Kipchumba, ndio washindi wa makala ya mwaka huu ya mbio za nusu marathaoni za The Great North Run, zilizoandaliwa Jumapili nchini Uingereza.
Ngugi alishinda mbio za wanawake akiziparakasa kwa saa 1 dakika 7 na sekunde 40,akifuatwa na Wahabeshi Senebere Teferi kwa saa 1 dakika 7 na sekunde 41, na Alemu Mergetu sekunde mojabaadaye katika nafasi za pili na mtawalia.
Mkenya mwingine Sheila Chepkirui alimaliza wa nne.
Kipchumba alishinda mbio za wanaume kwa kutumia muda wa dakika 59 na sekunde 52.