Home Biashara Wakenya kuruhusiwa kuondoa akiba kwenye Hustler Fund

Wakenya kuruhusiwa kuondoa akiba kwenye Hustler Fund

0

Wakenya ambao wamekuwa wakiomba mikopo na kuwekeza kwenye jukwaa la serikali la Hustler Fund wataanza kutoa akiba zao Novemba mwaka huu.

Waziri wa vyama vya ushirika, biashara ndogo na za kadri Simon Chelugui anasema kufikia sasa, wakenya wamewekeza shilingi bilioni 1.8 kwenye Hustler Fund.

Mikopo iliyotolewa kwenye jukwaa hilo lililoanzishwa na Rais William Ruto Novemba 2022 ni bilioni 36.

Kila mmoja anaweza kutoa asilimia 30 pekee ya jumla ya akiba yake Novemba Mosi.

Waziri Chelugui alihimiza wakenya wengine kujisajili kwenye jukwaa hilo la mikopo serikali inapojiandaa kuondoa mahitaji mengi Ili kuruhusu watu wengi zaidi kukopa.

Kulingana naye watakaokopa na kulipa kwa wakati watatambuliwa na serikali na kupendekezwa kwa mashirika mengine makubwa ya mikopo ambapo wanaweza kukopa pesa nyingi zaidi za kustawisha biashara zao.

Chelugui alitaja Hustler Fund kuwa jukwaa la mikopo la mkenya wa kawaida ambalo litasaidia wale ambao walikuwa wameharibu sifa zao za mikopo kujijenga tena.

Website | + posts