Home Habari Kuu Wakenya kupata vitambulisho vipya vya kidijitali

Wakenya kupata vitambulisho vipya vya kidijitali

0

Wakenya watapatiwa vitambulisho vipya vya kidijitali huku idara ya uhamiaji na kutoa huduma kwa wananchi ikianza kutekeleza agizo la Rais William Ruto la mwezi Juni.

Katibu wa idara hiyo Julius Bitok anasema watatekeleza hilo katika siku 90 zijazo na Wakenya watakuwa na vitambulisho hivyo kufikia mwezi Februari mwakani.

Katika usajili huo, taarifa muhimu za wananchi kama zilivyo kwenye sajili kuu zitanakiliwa na hatimaye zitasaidia serikali katika kuweka mikakati ya kugawa raslimali na kutoa huduma kwa Wakenya.

Kulingana na Bitok, mfumo huo mpya wa usajili una vipengele vinne ambavyo ni nambari maalumu ya utambuzi inayojulikana kama Maisha Namba, kadi ya utambulisho kidijitali inayojulikana kama Maisha kadi ambayo ni aina mpya ya kitambulisho cha kisasa cha kitaifa na kadi ya kidijitali ambayo inaweza kuhifadhiwa kwenye rununu.

Kipengee cha nne ni sajili kuu ya kitaifa ambayo itawajumlisha watu wote wanaoishi nchini Kenya wakiwemo wakimbizi.

Website | + posts