Home Kaunti Wakazi washauriwa kukata miti isiyo thabiti karibu na nyumba Nyandarua

Wakazi washauriwa kukata miti isiyo thabiti karibu na nyumba Nyandarua

Serikali ya kaunti ya Nyandarua imeshauri wakazi wa kaunti hiyo wakate miti ambayo inaonekana kuegemea upande na ambayo imekuwepo kwa miaka mingi karibu na nyumba zao na karibu na maeneo ya umma kama vile shule ili kuepusha hatari ambayo huenda ikasababishwa na mvua ya El Nino na upepo mkali.

Imeshauri wadau kushirikiana na kulainisha juhudi zao katika kuzuia athari ambazo huenda zikatokana na mvua kubwa inayotarajiwa ya El’Nino.

Kundi la maafisa wa serikali kuu na serikali ya kaunti ya Nyandarua la kushughulikia maandalizi ya mvua ya El Nino lilifanya mkutano mjini Ol Kalou. Wanachama wa kundi hilo walisisitiza umuhimu wa wakazi kutambua hatari inayotokana na miti iliyokua kupita kiasi.

Mtunzaji mkuu wa misitu katika kaunti ya Nyandarua, John Njoroge, alihimiza wakazi kutumia fursa ya mvua hiyo kupanda miti kwa wingi.

Peter Wambugu,mkurugenzi wa idara ya utabiri wa hali ya hewa katika kaunti ya Nyandarua alisema mvua hiyo kubwa inatarajiwa kuanza wiki ya kwanza au ya pili ya mwezi huu wa Oktoba.

Wakazi wanahimizwa kuwa waangalifu na kuepuka maeneo yaliyo chini wakati wa mvua hiyo.

Website | + posts
Lydia Mwangi
+ posts