Home Kaunti Wakazi wa Rurii kaunti ya Nyandarua walalamikia ongezeko la matumizi ya pombe...

Wakazi wa Rurii kaunti ya Nyandarua walalamikia ongezeko la matumizi ya pombe na mihadarati

Wakazi wa wadi ya Rurii katika kaunti ya Nyandarua wamelalamikia kile wanachokitaja kuwa ongezeko la matumizi ya pombe na mihadarati katika eneo hilo huku wakilaumu afisa mmoja wa serikali anayesimamia eneo hilo kwa kukubalia uuzaji wa pombe haramu.

Hali hiyo imesababisha viongozi kadhaa wa kaunti ya Nyandarua kupaaza sauti akiwemo mwakilishi wa kike wa kaunti hiyo bungeni Faith Gitau.

Gitau aliitaka serikali ya kaunti kuwajibika kwa sababu biashara nyingi haramu zinaendeshwa chini ya uangalizi wake na hakuna hatua iliyochukuliwa hata baada ya miito kutoka kwa serikali kuu kuhusu vita dhidi ya matumizi ya pombe haramu.

Gitau aliambatanisha ongezeko na utengenezaji wa pombe haramu na kuzembea kwa serikali ya kauti na watekelezaji sheria wafisadi ambao wanasemekana kuwakinga wahusika wa utengenezaji na uuzaji wa pombe haramu.

Mbunge huyo sasa anamtaka Gavana Kiarie Badilisha kukoma kutoa leseni na kutekeleza msako kwenye maeneo yote ya kuuza pombe katika kaunti hiyo.

Gitau aligusia pia haja iliyopo ya kuimarisha sekta ya afuya katika kaunti hiyo kwa kutoa vifaa hitajika kwa zahanati zote.

Kulingana naye, vituo vingi vya afya katika kaunti ya Nyandarua havina dawa, madaktari wa kutosha na miundomsingi suala linalolazimu wakazi kusafiri mbali kutafuta huduma za afya.

Website | + posts
Lydia Mwangi
+ posts