Home Kaunti Wakazi wa Moa, Lamu walalamikia uteuzi wa Chifu

Wakazi wa Moa, Lamu walalamikia uteuzi wa Chifu

0

Wakazi wa eneo la Moa katika kaunti ya Lamu wamelalamikia mchakato wa kuteua chifu wa eneo hilo wakisema haukuwa wa haki.

Wakiongozwa na Bonea Boru, wakazi hao walizungumzia kutoridhika kwao wakisema mpango mzima wa uteuzi ulikosa haki na uwazi kwani jamii haikuhusishwa.

Pia wanadai kwamba uteuzi huo haukufuata kanuni zilizoko za uteuzi.

Kulingana nao, mchakato wa uteuzi huo ulionekana kama ambao ulipendelea watu fulani na haukuwa jumuishi ili maoni na maslahi ya jamii nzima yazingatiwe.

Sultan wa kaunti ya Lamu Omar Sharif ametoa makataa ya siku saba kwa serikali itangaze upya nafasi hiyo kuwa wazi ili mchakato mzima wa uteuzi urudiwe.

Alisema iwapo serikali haitatekeleza matakwa yao, yeye na wakazi wa eneo la Moa watakwenda mahakamani kutafuta haki na kusimamisha naibu chifu aliyeteuliwa asihudumu.

KBC Digital
+ posts