Home Kaunti Wakazi wa Milimani, Kakamega walalamikia bomoabomoa

Wakazi wa Milimani, Kakamega walalamikia bomoabomoa

0
Baadhi ya wakazi walioagizwa na serikali kuhama makazi yao sehemu ya Milimani mjini Kakamega ili kupeana nafasi ya ujenzi wa nyumba za nafuu na wameilaumu serikali kwa kuendelea kuwatatiza kwa kubomoa nyumba zao nyakati za usiku.
Wakazi hao wanadai walipewa mashamba hayo na aliyekuwa Rais wa nchi marehemu Daniel Moi.
Zoezi la bomoabomoa lililoanza wiki iliyopita linasemekana kufanyika usiku, jambo ambalo wanasema ni kinyume cha sheria wakati wanapopaswa kupewa notisi kabla ya zoezi hilo kuendelea.
Wanashangaa kuona dhuluma hizo zinaendelea licha ya serikali za awali kutowahi kuwasumbua, na wanajiuliza sababu za kuendelea kuteseka huku wakiwa na kibali cha mahakama kinachozuia bomoabomoa hiyo kuendelea.
Kwa sasa wanaendelea kuishi kwa hofu wasijue mahali pa kupata haki na kilio chao kusikizwa.
Carolyn Necheza
+ posts