Home Kaunti Wakazi wa Meru wamtaka Gavana Mwangaza kuondoka mamlakani

Wakazi wa Meru wamtaka Gavana Mwangaza kuondoka mamlakani

Wakati wa maandamano hayo, baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi ya Meru waliathiriwa na vitoa machozi vilivyorushwa ndani ya shule hiyo.

0
Wakazi wa Meru waandamana.
kra

Wakazi wa kaunti Meru leo waliandamana kushinikiza kuondoka afisini kwa Gavana wa kaunti hiyo Kawira Mwangaza.

Wakati wa maandamano hayo, baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi ya Meru waliathiriwa na vitoa machozi vilivyorushwa ndani ya shule hiyo.

kra

Licha ya mahakama kufutilia mbali hatua ya bunge la Senate kumbandua gavana huyo, wakazi wa Meru wanashikilia kuwa, Mwangaza yuko afisini kinyume cha sheria.

Awali bunge la kaunti ya Meru, lilipiga kura kumtimua Gavana huyo kwa madai ya ukiukaji wa katiba, utumizi mbaya wa mamlaka na utovu wa nidhamu.

Bunge la Senate lilidumisha kutimuliwa kwa Gavana huyo, baada ya bunge lote kusikiliza na kupigia kura mashtaka dhidi ya Kawira.

Hata hivyo, saa chache baadaye Gavana huyo kupitia mawakili wake, walipinga hatua ya kumtimua mahakamani.

Mahakama kuu ilibatilisha kutimuliwa kwa Kawira, na kumpa afueni ya kuendelea kuhudumu hadi kesi aliyowasilisha itakaposikizwa na kuamuliwa.

Website | + posts
Jeff Mwangi
+ posts