Home Biashara Wakazi wa Meru: Gharama ya maisha ingali juu

Wakazi wa Meru: Gharama ya maisha ingali juu

0
kra

Siku chache baada ya Waziri wa Kilimo Mithika Linturi kuonekana akizuru supamaketi mbalimbali jijini Nairobi kubaini bei ya bidhaa mbalimbali za vyakula hasa unga, Wakenya wengi bado wameelemewa na gharama ya juu ya maisha.

Wakati wa ziara zake, Linturi alisema bei ya unga imepungua.

kra

Hata hivyo, Favored Gakii, mkazi wa kaunti ya Meru anasema familia nyingi hazina chakula kwani hali imekuwa si hali tena kutokana na gaharama ya juu ya maisha.

Anasema kwa sasa, Wakenya wengi wanafanyia kazi matumbo yao tu na kuitaka serikali kuwazia kupunguza gharama ya vyakula.

Gakii anasema hata msimu huu wa Krismasi, Wakenya wengi hawatasherehekea walivyotarajia kutokana na gharama ya juu ya maisha.

Katika supamaketi ya Bei Sawa katika eneo la Makutano mjini Meru, tulikutana naye Sammy Macharia, meneja wa tawi hilo.

Alituambia kuwa kama wafanyabiashara, wanalazimika kupunguza gharama ya bidhaa hasa vyakula kwani wanataka kudumisha wateja wao.

Macharia anasema serikali inapaswa kufikiria kupunguza baadhi ya ushuru ili Wakenya waweze kumudu bei ya baadhi ya bidhaa muhimu kama vile vyakula na kuwaelimisha watoto wao.

Ashir Ondoyo ni mfanyakazi katika supamaketi hiyo. Anasema wengi wa wanawake wamesahau juu ya urembo wao kwani ni wachache wanaoweza kustahimili bei ya vipodozi vinavyouzwa katika supamaketi hiyo.

Alisema gharama ya juu ya ushuru thamani wa ziada, VAT kwenye vipodozi imewafanya wanawake wengi kukoma kununua vipodozi na kuazimia kununua bidhaa za vyakula kutokana na gharama ya juu ya maisha.

Jeff Mwangi
+ posts