Home Kaunti Wakazi wa Machakos wafaidi kutokana na kambi ya matibabu bila malipo

Wakazi wa Machakos wafaidi kutokana na kambi ya matibabu bila malipo

Zaidi ya wakenya alfu tatu walipokea matibabu na vipimo bila malipo katika kaunti ya machakos katika kambi ya matibabu kwa wananchi iliyoandaliwa na kampuni ya safaricom kupitia mpango wa wakfu wa M-pesa, katika kijiji cha vota.

Katika hafla hiyo iliyoudhuriwa na waziri wa afya wa kaunti ya machakos Daniel yumbya na baadhi ya wasimamizi wa wakfu wa M-pesa wakenya walieleza manufaa waliyopata kutokana na mpango huo wa kupimwa na tutibiwa bila malipo

Wengi walisifia hatua hiyo kama inayowapa fursa ya kupata matibabu na vipimo ambavyo kwa kawaida huwa ghali mno kwa mkenya wa maisha ya chini.

Akizungumza kwenye hafla hiyo waziri Daniel Yumbya alisema kwamba waliopatikana na maradadhi kutokana na vipimo vya jana watapokea matibabu bila malipo katika hospitali za kaunti ya machakos.

Aidha wito umetolewa kwa wakenya kujitokeza kwa wingi kupata vipimo mbalimbali nchini ili kuzuia vifo vya ghafla ambavyo husababishwa na magonjwa kama shinikizo la damu na maradhi mengine ambayo hayana dalili mwilini mapema.

Baadhi ya vipomo walivyofanyiwa wananchi ni pamoja na mpigo wa moyo, shinikizo la damu, viwango vya sukari mwilini,saratani miongoni mwa vingine.

Website | + posts
Jonathan Mutiso
+ posts