Mamia ya wakazi wa maeneo ya Ngomeni na Mandongoi, eneo la Mwingi Kaskazini kaunti ya Kitui, wametoroka makwao kwa hofu ya usalama kufuatia uvamizi unaofanywa na wezi wa mifugo waliojihami.
Mwanafunzi mmoja wa darasa la saba alipigwa risasi na wezi wa mifugo na kujeruhiwa alipokuwa akichunga mifugo wikendi iliyopita na nyumba kadhaa kuteketezwa.
Pia jumla ya watu watano waliuawa katika kipindi cha juma moja lililopita, hali ambayo imewafanya wakazi kutoroka.
Kina mama na watoto wameonekana wakihama na mizigo yao kukimbilia usalama kwa kuhofia uvamizi zaidi.