Home Habari Kuu Wakazi Uasin Gishu waandamana kulalamikia pombe haramu

Wakazi Uasin Gishu waandamana kulalamikia pombe haramu

Kulingana na wanawake hao, unywaji huo wa pombe haramu umesababisha maafa hasaa miongoni mwa vijana.

0
Wakazi waandamana kulalamikia Pombe haramu Uasin Gishu.

Wanawake walishiriki maandamano leo Alhamisi katika eneo bunge la Moiben kaunti ya Uasin Gishu, kulalamikia ongezeko la unywaji pombe haramu.

Kulingana na wanawake hao, unywaji huo wa pombe haramu umesababisha maafa hasaa miongoni mwa vijana.

Wanawake hao waliokuwa wakiandamana katika soko la Garage, walisema vijana tisa walipoteza maisha yao baada ya kubugia pombe hiyo mwezi uliopita.

Akina mama hao waliandamana wakibeba mabango na matawi ya miti huku wakipaza sauti zao wakiomba serikali ya kaunti ya Uasin Gishu kufunga baa katika soko la Garage ambazo zimekuwa kero kwa familia sababu ya ulevi uliokithiri.

Soko hilo la Garage lina baa takriban 25 zilizo na leseni, huku zingine zikiendesha biashara bila leseni.

Wanawake hao walihusika katika makabiliano mafupi na baadhi ya walevi lakini polisi waliingilia kati na kuzuia kuzuka kwa vurugu.

Naibu wa Kamishna wa kaunti hiyo Noela Diffu, alifika eneo hilo la Garage na kuwatuliza wanawake hao waliojawa na ghadhabu.

Diffu alisema jamii ya eneo hilo imetuma ombi kwa serikali ya kaunti kufunga baa na maeneo ya unywaji pombe haramu katika eneo hilo.

“Kwa kuwa sasa tuna majina ya wahusika nitapeleka mbele malalamishi yenu ili hatua zichukuliwe mara moja”, alisema naibu huyo.

Kaimu OCPD eneo hilo Kariuki Ndegwa alisema watashirikiana na mashirika yote husika kukabiliana na ulevi wa kupindukia eneo hilo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here