Home Vipindi Wakazi Nyandarua waandamana, walalamikia barabara mbovu

Wakazi Nyandarua waandamana, walalamikia barabara mbovu

0
kra

Wakulima na wakazi wa kijiji cha Nyakariang’a eneo la Ndunduri kaunti ya Nyandarua wameandamana kulalamikia barabara mbovu.

Wameitaka serikali kupitia viongozi waliochaguliwa kuwashughulikia kwa kuijenga wakisema mazao yao yanaozea mashambani na hali ya usafiri ni tata.

kra

Wakizungumza baada ya kuandamana, wakazi hao ambao wengi ni wakulima wameitaka serikali kuishughulikia barabara hiyo ya zaidi ya kilomita 20 ili waweze kuwa na wakati rahisi kutoa mazao yao shambani na kuyapeleka sokoni.

Wamelalama kuwa mazao yao yanaoezea mashambani na maziwa kuharibikia manyumbani.

Aidha wakulima hao wanawataka viongozi waliochaguliwa kuingilia kati na kuhakikisha barabara hiyi ambayo ilikuwa inajengwa na serikali na kusimama kwa muda wa miaka mitatu inaangaziwa na kukamilishwa.