Home Habari Kuu Wakazi Machakos wafunga barabara iliyo na vumbi jingi

Wakazi Machakos wafunga barabara iliyo na vumbi jingi

0

Usafiri ulitatizwa kwa muda kwenye barabara ya Devki – Kinanie – Joska katika kaunti ya Machakos baada ya wakazi wa eneo hilo kuandamana na kuifunga katika soko la Kinanie.

Wakazi hao ambao walijumuisha wafanyabiashara, wakazi na wanaoendesha bodaboda walikabiliana na maafisa wa polisi huku wakilalamikia vumbi jingi ambalo wamesema ni hatari kwa afya yao.

Barabara hiyo inaunganisha barabara ya Mombasa na ile ya Kangundo na ilifungwa kwa zaidi ya saa 10 na kutatiza madereva wa malori ambao huitumia kusafirisha vifaa vya ujenzi na malighafi ya kutengeneza saruji kwa viwanda vilivyoko Athi River.

Walisema ujenzi wa barabara hiyo ulianzishwa miaka miwili iliyopita lakini kwa sasa umesitishwa.

Wengi kati ya waandamanaji hao walipata majeraha madogo madogo kutokana na hali ya kukimbizana na maafisa wa polisi ambao walitumia vitoza machozi kuwatawanya.

Mwakilishi wa wadi ya Kinanie Francis Kavyu alijipata kwenye vurumai hiyo alipoelekea eneo la maandamano baada ya kujuzwa. Gari lake lilirushiwa vitoza machozi.

Watu hao zaidi ya 2,000 sasa wanataka serikali ichukue hatua ya kutengeneza barabara hiyo muhimu ambayo imekuwa kero kwao.

Ripoti yake Anthony Musyoka

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here