Home Habari Kuu Wajumbe wa UDA walalamikia kuahirishwa kwa uchaguzi wa Nairobi

Wajumbe wa UDA walalamikia kuahirishwa kwa uchaguzi wa Nairobi

0
kra

Siku moja baada ya chama cha United Democratic Alliance kuahirisha uchaguzi katika kaunti ya Nairobi, wafuasi wa mbunge wa Embakasi Kaskazini James Gakuya na wale wa Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja, walifurika katika afisi cha chama hicho kulalamikia hatua hiyo.

Gakuya na Sakaja wanawania wadhifa wa mwenyekiti wa chama cha UDA katika kaunti ya Nairobi.

kra

Wajumbe hao walifika katika afisi za UDA zilizoko katika barabara ya Ngong, kuelezea kutoridhika kwao na hatua ya kuahirisha uchaguzi huo dakika za mwisho.

Siku ya Ijumaa chama cha UDA kupitia kwa taarifa, kiliahirisha uchaguzi katika kaunti ya Nairobi, uliokuwa uandaliwe leo Jumamosi katika ukumbi wa Bomas of Kenya.

“Kutokana na sababu ambazo haziwezi epukika, uchaguzi katika kaunti ya Nairobi hautafanyika jinsi ilivyopangwa,” ilisema taarifa iliyotiwa saini namwenyekiti wa kitaifa wa bodi ya uchaguzi.

Hii ni mara ya tatu kwa uchaguzi huo kuahirishwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here