Home Kaunti Wajibikeni la sivyo niwapige kalamu, Gavana Ayacko awaonya mawaziri wake

Wajibikeni la sivyo niwapige kalamu, Gavana Ayacko awaonya mawaziri wake

0
Gavana wa Kaunti ya Migori Ochillo Ayacko ametoa onyo na tahadhari kwa baraza lake la mawaziri ambao wana uraibu wa kuzembea kazini na kulemaza shughuli na miradi ya maendeleo Kwa mwanachi wa kawaida.
Akizingumza katika hafla ya kusaini mikataba ya utendakazi baina ya serikali ya kaunti ya Migori na mawaziri hao, Ayacko alieleza kuwa ni lazima mawaziri hao wahakikishe wamezingatia na kutimiza malengo yake kama ilivyoratibiwa katika manifesto yake wakati wa kampeni.
Alisema hawana budi kufikisha maendeleo hadi mashinani kwani yeyote ambaye atapatikana akidhalilisha mpiga kura katika kaunti hiyo atapigwa kalamu.
Gavana huyo alieleza kuwa mkataba kati ya Baraza la Mawaziri na serikali ya kaunti ya Migori itakuwa ikisainiwa kila baada ya mwaka mmoja kama njia mojawapo ya kuhakikisha utendakazi bora kwa wakazi wa kaunti hiyo.