Waislamu kote nchini Kenya wamejumuika katika maeneo ya kuabudu kusherehekea sikukuu ya Eid- Eil- Adha.
Siku hiyo husherehekewa kwa kuchinja mifugo na kugawana na wasiobahatika katika jamii na ni kumbukumbu ya Mtume Mohammed kuwa tayari kumtoa kafara mwanawe Ismail.
Siku hiyo ni mojawapo ya sikukuu katika kalenda ya Waislamu ambao huchinja mbuzi au kondoo na kula pamoja na wasiojiweza katika jamii baada ya ibada.