Home Biashara Waiguru: Mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Kenya na EU utafaidi...

Waiguru: Mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Kenya na EU utafaidi wakulima

0

Mwenyekiti wa Baraza la Magavana Anne Waiguru amepongeza kutiwa saini kwa mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Kenya na Umoja wa Ulaya, EU. 

Mkataba huo ulitiwa saini leo Jumatatu katika Ikulu ya Nairobi wakati wa hafla iliyohudhuriwa na Rais William Ruto na Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen.

Waiguru ambaye pia ni Gavana wa Kirinyaga ametaja hatua hiyo kuwa muhimu kwa wakulima, kaunti na taifa la Kenya kwa jumla.

“Huku tukiongeza uzalishaji katika mashamba yetu na kuanzisha vyama vya ushirika katika kaunti kupitia mitungo maalum ya thamani na uongezaji thamani, tunapongeza fursa hii ya kupanua ushiriki wetu katika biashara ya dunia na kuongeza mapato ya wakulima wetu,” alisema Waiguru.

“Ni fahari kwa Baraza la Magavana kuwa sehemu ya safari hii ya mabadiliko na CAIPS na EPZ.”

Mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Kenya na EU uliafikiwa baada ya mashauriano ambayo yalikamilika Juni 19, 2023.

Unalenga kuimarisha biashara ya bidhaa na kubuni fursa mpya za kiuchumi, ushirikiano unaolenga kupiga jeki ukuaji wa kiuchumi wa taifa la Kenya.

Baadhi ya mambo yaliyo kwenye mkataba huo ni kufunguliwa kwa masoko ya EU kwa bidhaa za Kenya, kumotisha uwekezaji wa EU nchini Kenya, kusimamiaA biashara thabiti na endelevu, kuweka masharti thabiti kuhusu masuala ya leba, usawa wa kijinsia, utunzaji wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Website | + posts