Home Habari Kuu Wahudumu wa matatu watakiwa kujiepusha na mihadarati

Wahudumu wa matatu watakiwa kujiepusha na mihadarati

Mke wa naibu Rais kasisi Dorcas Rigathi, alisema sekta ya matatu haipaswi kupuuzwa.

0

Wahudumu wa matatu wamehimizwa kujiepusha na utumizi wa pombe na mihadarati, kwani zinasababisha changamoto nyingi katika familia changa.

Mke wa Naibu Rais Dorcas Rigathi amesema sekta ya matatu haipaswi kupuuzwa kwa kuwa inatekeleza wajibu muhimu katika jamii.

Dorcas aliyasema hayo katika kaunti ya Kisii, alipozindua kambi ya siku mbili ya matibabu inayowalenga wahudumu wa matatu na wale walioathiriwa na utumizi wa mihadarati katika juhudi zake za kumuinua mtoto wa kiume.

Kambi hiyo ya matibabu pia inalenga familia zinazoishi mitaani katika kaunti ya Kisii.

Kasisi Dorcas Rigathi azindua Kambi ya matibabu Kwa wahudumu wa matatu.

“Madereva na utingo wa matatu na wengine katika sekta ya matatu, wanapaswa kuheshimiwa kama sehemu ya wanaochochea ukuaji wa uchumi. Wengi wetu tunawathamini na maisha yetu, lakini hatuheshimu kazi yao. Nitatembea nanyi,” alisema Dorcas.

Gavana wa Kisii Simba Arati kwa upande wake alipongeza juhudi za mkewe Naibu Rais za kumuinua mtoto wa kiume akisema hatua hiyo inasaidia pakubwa kuokoa kizazi kilichoko.

Dorcas Rigathi yuko katika kaunti ya Kisii kwa ziara rasmi ya siku tatu.

Website | + posts