Home Kaunti Wahasiriwa wa mafuriko Tana Delta wapinga uamuzi wa kuwaondoa kambini

Wahasiriwa wa mafuriko Tana Delta wapinga uamuzi wa kuwaondoa kambini

0

Baadhi ya walioathirika kutokana na mafuriko na ambao wamekuwa wakiishi katika kambi ya wakimbizi ya Minjila wamepinga hatua ya serikali ya kujaribu kuwahamisha kutoka ardhi yao.

Wahasiriwa hao wanaojumuisha kaya 350 na kutoka vijiji vya Danisa na Onkoldhe ambavyo vilizamishwa na maji, pia walidai kuwa serikali ya kaunti ilikata usambazaji wa maji katika kambi hiyo kama njia ya kuwalazimisha kuondoka eneo hilo.

Baadhi ya waathiriwa walielezea hofu kwa vile hawajui ni lini serikali ya kaunti itawafurusha na hawana mahali pa kuhamia.

Wahasiriwa hao walipiga kambi kwa mara ya kwanza katika eneo hilo mwaka jana wakati wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua ya El Nino na kufikia mwaka huu, mafuriko ya sasa yamewahamisha tena.

Sasa wanatoa wito kwa serikali kusitisha mipango yoyote ya kuwahamisha na kuwatafutia mahali mbadala kwa kuwa hawataki kurejea katika kitongoji hicho ambacho kinakumbwa na mafuriko.

Jemie Saburi
+ posts