Home Taifa Wahandisi wahimiza ujumuishaji katika kuboresha JKIA

Wahandisi wahimiza ujumuishaji katika kuboresha JKIA

0
kra

Wahandisi wa humu nchini sasa wanapendekeza kwamba mbinu jumuishi itumike katika mchakato mzima wa kuboresha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, JKIA.

Katika taarifa ya kina iliyotiwa saini na Rais wa Chama cha Wahandisi nchini, IEK Shammah Kiteme, wahandisi wanahisi kwamba usafiri wa angani ni muhimu katika taifa hili.

kra

Takwimu walizotoa kwenye taarifa hiyo zinaashiria ukuaji wa sekta hiyo ikitizamiwa kwamba mnamo mwaka 2022, wasafiri  ndani ya nchi na wa kimataifa walifika milioni 10.2 kutoka kiwango cha milioni 6.5 kwa mwaka wakati wa janga la virusi vya korona.

Pendekezo la awamu tatu la kampuni ya kutoka India ya Adani ambayo inasemekana kupatiwa zabuni ya kuimarisha uwanja huo kulingana IEK halishughulikii changamoto zilizoko.

Wanahisi kwamba kampuni ya Adani inalenga fursa ambazo zinajitokeza katika usimamizi wa uwanja wa JKIA na wala sio changamoto.

Huku wakikubali kwamba uwanja huo unahitaji kuimarishwa ili kushindana vyema na viwanja vingine vya ndege katika kanda hii, wahandisi wanasema ni bora kuangazia changamoto hizo.

Changamoto hizo ni pamoja na nafasi ya kushughulikia ndege nyingi zinazotua kwenye uwanja huo, kuboreshwa kwa sehemu za kuabiri na kushuka ndege, kuboreshwa kwa mifumo ya kiufundi na kushughulikia kunyakuliwa kwa ardhi ya uwanja wa ndege.

Katika awamu ya kwanza mwaka 2024 hadi 2028, Adani inapendekeza kujenga jengo jipya la kuabiri ndege, barabara ya kuunganisha maeneo mawili ya kuabiri ndege, jengo la maegesho ya magari, hoteli kadhaa na kukarabati majengo yaliyoko.

Awamu ya pili mwaka 2029 hadi 2035 itakuwa ya uboreshaji wa maeneo ya maegesho ya teksi na ujenzi wa maegesho ya ndege.

Mwaka 2036 hadi 2054, kampuni ya Adani itapanua eneo kuu la uabiri ili liweze kushughulikia abiria milioni 8, itajenga maeneo zaidi ya maegesho ya ndege, kuboresha barabara za ndani na karibu na uwanja huo wa ndege pamoja na kuboresha mifumo mbalimbali inayotumika humo.

Website | + posts