Home Habari Kuu Wahamasishaji wa afya ya jamii waanza kupewa simu za smartphone

Wahamasishaji wa afya ya jamii waanza kupewa simu za smartphone

0

Serikali imeanza kuwapatia wahamasishaji wote 100,000 wa afya ya jamii simu za mkononi aina ya smartphone kuendana na ajenda ya afya ya dijitali. 

Ili kudhihirisha hilo, Waziri wa Afya Susan Nakhumicha leo Jumanne alisimamia usambazaji wa simu hizo katika hospitali ya J.M Kariuki katika kaunti ya Nyandarua.

Simu hizo zinakusudia kuboresha upatikanaji wa wahamasishaji wa afya ya jamii na ubadilishanaji wa data na kwa misingi hiyo kupunguza mzigo kwa wale wanaotafuta huduma za afya ya msingi.

Kulingana na Waziri Nakhumicha, mpango huo unapiga jeki juhudi za kuhakikisha upatikanaji wa afya kwa wote kama ilivyoelezwa na Rais William Ruto wakati wa sherehe za mwaka huu za siku ya Mashujaa zilizoandaliwa katika kaunti ya Kericho.

Utawala wa Kenya Kwanza umezindua wahamasishaji wa afya ya jamii 100,000 huku ikitazamiwa kwamba kila mmoja atahudumia kaya 100.

Wahamasishaji hao wamepatiwa vifaa tiba vya kisasa ili kusaidia kuwahudumia ipasavyo raia mashihani.

Website | + posts