Home Habari Kuu Waganga wakamatwa Tanzania kwa kuhudumu bila vibali

Waganga wakamatwa Tanzania kwa kuhudumu bila vibali

0
Theopista Mallya mkuu wa polisi mkoani Songwe, Tanzania
kra

Maafisa wa polisi nchini Tanzania wametangaza kwamba wamekamata watu 11 kwa tuhuma za kuendesha shughuli za uganga wa kienyeji bila vibali.

Kwenye oparesheni iliyofanywa Januari 9, 2024 katika mkoa wa Songwe, Mwene Nzunda wa umri wa miaka 44, Anthony Yatilinga Mapumba wa umri wa miaka 65, Isambi Yasinta Mghallah wa miaka 80, Ngawelo Mziho wa miaka 53 na Tamimu Ballison Mdolo wa miaka 57 walikamatwa.

kra

Wengine ni Biton Daimon Nzunda wa miaka 64, Amos Nzunda wa miaka 23, Stephen Mwilenga wa miaka 46, David Frank Mapumba 72, George Greyson Mghallah wa miaka 43 na Jailos Sola wa umri wa miaka 42.

Polisi wanasema wanaendeleza uchunguzi dhidi ya washukiwa hao na watafunguliwa mashtaka hivi karibuni.

Wakazi wa mkoa wa Songwe wanakumbushwa na polisi kwamba ni marufuku kwa yeyote kuendesha shughuli za uganga bila kibali ikiwa ni pamoja na kitendo cha kusafisha nyumba zinazodhaniwa kuwa na uchawi.

Wanakumbushwa pia kwamba yeyote anayeandaa mkutano wa aina yoyote ni lazima afahamishe viongozi wa eneo.