Home Habari Kuu Wafungwa wa 85 wa Ethiopia walio gerezani Kajiado wasusia chakula

Wafungwa wa 85 wa Ethiopia walio gerezani Kajiado wasusia chakula

0

Wafungwa 85 raia wa Ethiopia walio katika gereza la Illasit, kaunti ya Kajiado wakisubiri kurejeshwa nyumbani  wamesusia chakula.

Wafungwa hao, wakiwemo wanaume na wanawake, walikamatwa na polisi  tarehe 20 mwezi huu na kupelekwa katika mahakama ya Loitoktok iliyoamrisha kurejeshwa kwao nchini Ethiopia.

Polisi wanasema raia hao walipatikana wamefungiwa katika  chumba kimoja ambacho mwenyewe hajabainika, na yamkini walikuwa katika safari ya kuelekea nchini Afrika Kusini kutafuta kazi.

Watoro hao wameapa kususia chakula hadi warejeshwe kwao, hatua ambayo imesababisha wao kuwa wadhaifu.