Home Habari Kuu Wafanyakazi wa Posta waanza mgomo

Wafanyakazi wa Posta waanza mgomo

0

Wafanyakazi wa shirika la Posta nchini wameanza mgomo rasmi siku ya Alhamisi, baada ya serikali kushindwa kutimiza matakwa yao kufikia Novemba mosi.

Wafanyakazi hao zaidi ya 2,000 wanadai malimbikizi ya mshahara wa miezi mitano.

Kulingana na katibu kmuu wa chama cha wafanyakazi wa sekta ya mawasiliano Benson Okwaro, watasitisha mgomo punde tu wafanyakazi hao watakapolipwa.

Wafanyakazi hao pia wanataka kulipwa kwa matozo yote ya lazima kama vile NSSF, NHIF, mikopo ya benki na vyama vya ushirika.