Home Habari Kuu Wafanyakazi wa Posta watangaza mgomo kuanzia Novemba wakidai mshahara wa miezi saba

Wafanyakazi wa Posta watangaza mgomo kuanzia Novemba wakidai mshahara wa miezi saba

0

Wafanyakazi wa shirika la Posta nchini wametoa ilani ya wiki mbili ya mgomo wa kitaifa kutaka walipwe malimbikizi ya mshahara wa miezi sita kuanzia mwezi Juni mwaka huu.

Akizungmza na wanahabari mapema Jumapili, Katibu Mkuu wa shirika la wafanyakazi wa sekta wa ya mawasiliano nchini, COWU Benson Okwaro amesema wanataka shirika la Posta nchini kulipa malimbikizi ya mshahara wa miezi sita pamoja na mshahara wa mwezi huu na matozo ya lazima kama vile ya vyama vya ushirika,mikopo ya benki na hazina ya kustaafu kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita ifikiapo tarehe 30 mwezi huu, la sivyo wafanyakazi watagoma kuanzia Novemba 2.

Okwaro pia anaitaka serikali kuwalazimisha walio na madeni ya Posta ikiwemo shilingi bilioni 1.7 wanazodai vituo vya Huduma Centre kwa miaka mitano na shilingi bilioni 1.6 wanazodai Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini, IEBC tangu uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Okwaro anasema endapo madeni hayo yatalipwa, shirika la Posta litaweza kulipia mishahara na madeni yake yote.

Website | + posts