Home Biashara Wafanyakazi wa kampuni ya Boeing wagoma nchini Marekani

Wafanyakazi wa kampuni ya Boeing wagoma nchini Marekani

0
kra

Shughuli za kawaida katika kiwanda cha kampuni ya Marekani cha kuunda ndege aina ya Boeing, zimekwama Ijumaa baada ya wafanyakazi kususia kazi wakiteta kuhusu kandarasi za utendakazi.

Mgomo huo ni wa kwanza kwenye kampuni hiyo tangu mwaka 2008 ambayo imekuwa ikikashifiwa vikali na wateja pamoja na wanaodhibiti ndege, baada ya mlango wa ndege yake mmoja kuporomoka ikiwa angani katikati ya Januari mwaka huu.

kra

Bei ya hisa za kampuni hiyo pia zilishuka kwa asilimia nne Ijumaa kutokana na athari za mgomo huo.

Kampuni ya Boeing inakabiliwa na madeni ya dola bilioni 60 na mgomo wa hivi punde ni pigo kubwa .

Ilikuwa mara ya kwanza kwa wanyakazi hao kupiga kura ya kupinga ajira ya mkataba baada ya miaka 16, asilimia 94.6 wakipinga na pia asilimia 96 wakiunga mkono mgomo.

Wafanyakazi wa Boeing katika kiwanda cha Seattle kinachotengeneza ndege aina ya Boeing MAX 777 na 767 wamekuwa wakigoma tangu Jumatatu wiki hii.

Kulingana na takwimu, kampuni hiyo huenda ikapoteza dola bilioni 3 endapo wafanyakazi watagoma kwa siku 50.

Website | + posts