Home Kaunti Wafanyakazi wa bodi ya maji ya Lodwar (LOWASCO) wapokea mafunzo

Wafanyakazi wa bodi ya maji ya Lodwar (LOWASCO) wapokea mafunzo

0

Wafanyakazi wa bodi ya maji ya Lodwar, LOWASCO walinufaika kwa mafunzo ya kuboresha usimamizi na utendakazi.

Mafunzo hayo ya siku tatu kwa wafanyakazi wa halmashauri ya LOWASCO yalihusu mbinu za kisasa za usimamizi katika sekta ya maji.

Mafunzo hayo pia yalitoa fursa kwa wafanyakazi wa bodi hiyo kushauriana na maafisa wa bodi ya kudhibiti huduma za maji nchini, WASREB, chama cha watoa huduma za maji, WASPA na kampuni ya maji ya Eldoret, ELDOWAS.

Mafunzo hayo yalisimamiwa na shirika la The Ecovest Consultants wakiongozwa na Afisa Mkuu Mtendaji Isha Dunga.

Website | + posts