Home Biashara Wafanyakazi wa Mumias waitwa kampuni hiyo inaporejelea shughuli zake

Wafanyakazi wa Mumias waitwa kampuni hiyo inaporejelea shughuli zake

0

Watu zaidi ya 700 ambao walikuwa wafanyakazi wa kampuni ya sukari ya Mumias kabla ya kufungwa, wameitwa warejee kazini kampuni hiyo inaporejelea shughuli za kutengeneza sukari.

Stephen Kihumba, meneja wa shuguli na usimamizi wa kampuni hiyo anasema wafanyakazi zaidi wataitwa kurejea kazini siku chache zijazo.

Aliahidi kwamba wakulima watakaowasilisha miwa yao kwa kampuni hiyo watalipwa kila wiki lakini kampuni hiyo itasubiri kibali cha shirika la kukadiria ubora wa bidhaa kabla ya kuanza kuuza sukari itakayotengenezwa.

Wakulima watakuwa wakilipwa shilingi 6,050 kwa kila tani ya miwa suala ambalo limesababisha kampuni nyingine kuongeza malipo hayo kwa manufaa ya wakulima.

Kihumba alielezea pia kwamba kampuni ya Mumias imepanda miwa kwenye ekari 1,400 za shamba lake la ekari 3,400.

Kampuni ya Sarrai kutoka Uganda ndiyo inaendesha kampuni ya sukari ya Mumias chini ya mkataba wa miaka 20.

 

Website | + posts