Home Kimataifa Wafanyakazi wa afya kuanza mgomo katikati ya Julai

Wafanyakazi wa afya kuanza mgomo katikati ya Julai

0
kra

Vyama vya wafanyakazi wa afya vinashikilia kuwa vitaanza mgomo Julai 14, 2023 kutokana na kile kilivyotaja kuwa ukosefu wa hiari ya serikali kushiriki mazungumzo navyo juu ya mishahara yao. 

Wahudumu wa afya kupitia vyama vyao husika wanadai hata baada ya kuipa serikali muda wa kutosha kuangazia masuala yao kuhusiana makubaliano ya CBA, hawajaambulia chochote kutokana na nia yao njema.

kra

Akiwahutubia wanahabari leo Alhamisi, Katibu Mkuu wa Chama cha Matabibu, KUCO George Gibore alisema wafanyakazi wa afya tayari wamehangaishwa vya kutosha.

Vikitoa wito kwa sekta ya afya kupewa kipaumbele, vyama hivyo vinashinikiza kuajiriwa kwa wafanyakazi 20,000 wa afya kama ilivyoahidiwa na serikali.

Kadhalika vinaitaka serikali kuhusisha umma kuhusiana na namna ongezeko la michango ya Hazina ya Bima ya Kitaifa, NHIF itaboresha utoaji huduma kwa Wakenya.

Website | + posts