Home Habari Kuu Wadau wakutana Mombasa wakati kukiwa na mashaka ya Ukimwi

Wadau wakutana Mombasa wakati kukiwa na mashaka ya Ukimwi

0
Dkt. Ruth Laibon, Afisa Mkuu Mtendaji wa NSDCC (katikati) akiandamana na Dorothy Onyango (kushoto) na Prof. Ruth Nduati (kulia)
Dkt. Ruth Laibon, Afisa Mkuu Mtendaji wa NSDCC (katikati) akiandamana na Dorothy Onyango (kushoto) na Prof. Ruth Nduati (kulia)

Wataalam wameelezea wasiwasi kuhusiana na kuongezeka kwa visa vya maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi katika kaunti ambazo kwa kawaida zilikuwa na visa vichache. 

Waliyasema hayo kabla ya kuanza kuwa mkutano wa siku tatu wa washikadau mjini Mombasa kesho Jumanne uliopewa jina “Mkutano wa Maisha” unaolenga kuzifanya mapitio hatua zilizowekwa za kukabiliana na ugonjwa huo.

Akiwahutubia wanahabri kabla ya kuanza kwa mkutano huo, Dkt. Ruth Laibon ambaye ni ni Afisa Mkuu Mtendaji wa Baraza la Kitaifa la Udhibiti wa Magonjwa ya Kuambukizana (NSDCC) alidokeza kuwa changamoto ya kuchipuka kwa visa vya magonjwa ya mlipuko katika kaunti ambazo kwa kawaida hazikukumbwa na visa vya ugonjwa wa Ukimwi imeshuhudiwa katika kaunti kama vile Homa Bay.

Dkt. Laibon alisema wameshuhudia kuongezeka kwa visa katika kaunti kama vile Samburu, Mandera, na Garissa.

“Ingawa visa hivyo ni vichache, tuna mashaka kuwa ikiwa hatua hazitachukuliwa na watu kukosa kupata matibabu, basi vitageuka na kuwa changamoto,” alisema Dkt. Laibon.

Aliongeza kuwa viwango vya wanaume na wavulana kumeza dawa za ARV za kukabiliana na ugonjwa huo vipo chini zaidi ikilinganishwa na wanawake na wasichana ingawa ugonjwa wa UKIMWI umeenea sana miongoni mwa wanawake na wasichana.

“Tunawapoteza wanaume na wavulana wengi kutokana na Ukimwi kwa sababu hawafiki hospitalini mapema. Tunawapata tu katika kliniki za TB na nyakati nyingine wanapokuwa wagonjwa au wametumwa hospitalini kwa sababu ya nimonia na magonjwa mengine,” alielezea.

NSDCC inahamasisha kutambuliwa kwa magonjwa mapema miongoni mwa wanaume na wavulana ili kuzuia vifo vinavyohusiana na ugonjwa wa Ukimwi.

Dorothy Onyango aliyebainika kuambukizwa Ukimwi mnamo mwaka wa 1990 alisema nchi hii imepiga hatua katika kukabiliana na ugonjwa huo. Kupitia shirika lake linalojulikana kama “Women Fighting HIV in Kenya,” anakuza uelewa katika jamii.

“Kuna unyanyapaa mwingi katika jamii. Moja ya malengo yetu makuu ilikuwa namna ya kuuangamiza unyanyapaa huo,” alisema Dorothy.

Haniel Mengistu