Home Habari Kuu Wadau katika sekta ya ujenzi watakiwa kuzingatia maadili ya taaluma zao

Wadau katika sekta ya ujenzi watakiwa kuzingatia maadili ya taaluma zao

0
Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei
Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei

Kuna haja kwa wadau katika sekta ya ujenzi kuzingatia viwango vya juu vya uadilifu na utaalam katika utendakazi wao. 

Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei anasema hatua hiyo ni muhimu kwani kukosa kumakinika katika kazi zao husababisha madhara makubwa mno.

Kumekuwepo na visa visivyohesabika vya majengo kuanguka wakati wa ujenzi, visa ambavyo vimesababisha vifo na kuwaacha wengi wakiuguza majeraha katika sehemu mbalimbali nchini.

Visa ambavyo Koskei anasema vinapaswa kufikia kikomo.

“Taasisi katika sekta za ujenzi zinapaswa kutoa kipaumbele kwa hatua za kuzuia na kuepusha majanga kabla ya hatua za kukabiliana na uharibifu kuchukuliwa,” alisema Koskei wakati wa mkutano wa ushauri na wadau wa sekta hiyo.

“Wadau katika sekta ya ujenzi wanapaswa kupuuza maagizo yasiyokuwa halali kutoka mtu yeyote, ambayo yanaweza kuwafanya kupuuza maadili yao ya kitaaluma.”

Na ili kuepusha madhara yatokanayo wakati wa ujenzi, Mkuu wa Utumishi wa Umma sasa ametaka miradi yote ya serikali kupata leseni na idhini inayohitajika kabla ya kuanza kwa kazi yoyote ya ujenzi.

 

Website | + posts