Wacheza gofu chipukizi 22 wa Kenya wameanza mazoezi kujiandaa kwa mashindano ya kimataifa .
Timu hiyo itakita kambi ya mazoezi kaunzia wiki ijayo na inawajumuisha wavulana 12 na wasichana 10.
Wachezaji wanne kati ya walioitwa ni wale waliotamba wakati wa mashindano ya mwaliko ya NCBA kwa chipukizi maajuzi .
Wakati wa mashindano hayo Kanana Muthoni aliibuka mshindi katika kitengo cha wasichana kati ya umri wa miaka 11-12.
Mashindano ya NCA yaliyoandaliwa katika uwanja wa Muthaiga yaliwavutia washiriki 186 chipukizi.