Home Kaunti Wabunge wapendekeza kutimuliwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa NEMA

Wabunge wapendekeza kutimuliwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa NEMA

0

Kamati ya bunge la taifa kuhusu malalamishi ya umma, imependekeza kusimamishwa kazi kwa Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya kitaifa kuhusu  mazingira (NEMA) Mamo Boru Mamo, kwa kutoshughulia uchafuzi katika mto Athi.

Kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake mbunge wa Kitui Mashariki Nimrod Mbai, ilisema uchunguzi wa maji ya mto Athi, ulifichua matokeo ya kushangaza ya uchafuzi wa kemikali hatari zinazoweza kusababisha ugonjwa wa Saratani.

“Tumeangali hali ilivyo katika sehemu ya juu kunakotoka uchafuzi na sehemu ya chini ambako maji hayo yanatumiwa, na pendekezo letu la kwanza kama kamati ni kutimuliwa mara moja kwa mkurugenzi Mkuu wa NEMA, na majukumu yake yakabidhiwe mtu mwingine aliye na uwezo wa kuhakikisha usafi katika mto Tana ili watu wetu waache kufariki kutokana na saratani kila siku,” alifoka Mbai.

Aidha, alionya kwamba uchafuzi unaoendelea katika mto huo utadunisha umuhimu wa bwawa la Thwake lililogharimu mabilioni ya pesa kwani maji machafu kutoka mto huo huenda yakaingia bwawani humo.

Mbunge wa Baringo ya Kati, Joshua Kandie, ambaye pia ni mwanachama wa kamati hiyo; alipendekeza kutolewa kwa adhabu kali kwa wachafuzi wote wa mito humu nchini. Kamati hiyo ilizuru mto huo eneo la Mwala ambapo iliandaa kikao kupata maoni ya wakazi.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here