Home Taifa Wabunge wa Kenya Kwanza wakutana Ikulu

Wabunge wa Kenya Kwanza wakutana Ikulu

0
kra

Wabunge wa muungano unaotawala wa Kenya Kwanza wanakutana leo Jumanne asubuhi katika Ikulu ya Nairobi. 

Mkutano huo utaongozwa na Rais William Ruto na kuhudhuriwa na Naibu wake Rigathi Gachagua.

kra

Mivutano inayosemekana kushamiri kati yao inasemekana itakuwa miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa wakati Rais Ruto akifanya juhudi kuhakikisha meli ya serikali yake haizami.

Suala lingine linalotarajiwa kujadiliwa na Mswada wa Fedha 2024 ambao umeibua joto la kisiasa nchini kutokana na kile ambacho wengi wanasema utaongeza zaidi gharama ya maisha ikiwa utapitishwa.

Mswada huo unatarajiwa kuwasilishwa bungeni leo Jumanne na kamati ya fedha na mipango ya kitaifa inayoongozwa na mbunge wa Molo Kuria Kimani.