Baadhi ya wabunge wanaoegemea mrengo wa Azimio walitoka nje ya Bunge la Taifa Alhamisi alasiri muda mfupi baada ya Waziri wa Fedha Njuguna Ndung’u kusimama kusoma taarifa ya makadirio ya bajeti ya mwaka 2023/2024.
Licha ya wabunge hao kumzomea na kupiga kelele wakati wa kutoka, Waziri Ndung’u aliendelea kusoma bajeti kufuatia maelekezo ya Spika Moses Wetangula.
“Bajeti ya kumuumiza Mkenya mlalahoi hatutakubali,” alisema Mishi Mboko, mbunge wa Likoni baada ya kutoka nje ya bunge.
Kiongozi wa wachache Opiyo Wandayi aliongoza wabunge hao kutoka bungeni.