Home Taifa Wabunge kukamilisha kujadili Mswada wa Fedha 2024

Wabunge kukamilisha kujadili Mswada wa Fedha 2024

0
kra

Bunge la kitaifa linatarajiwa kukamilisha kujadili Mswada wa Fedha 2024 leo Alhamisi kabla ya kupiga kura Jumanne wiki ijayo.

Mswada huo wenye utata umezua tumbojoto huku Wakenya wengi wakihisi kuwa utaongeza ushuru na gharama ya maisha.

kra

Wabunge wengi wa upinzani wakiujadili mswada huo jana Jumatano, waliupinga wakisema haufai kwa wakati huu huku wabunge wanaoegemea serikali wakiuunga mkono.

Kulingana na Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula, wabunge wanapaswa kukamilisha mjadala wa mswada huo leo adhuhuri.

Awali, ilibidi serikali kuondoa baadhi ya vipengee katika mswada huo, ikiwemo ushuru wa magari wa asilimi 2.5 kila mwaka, ushuru thamani wa ziada wa asilimia 16 kwa mkate na ushuru kwa wanaotuma au kupokea hela kupitia kwa njia ya simu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here