Home Burudani Wabunge Betty Maina na Eric Wamumbi wafunga ndoa

Wabunge Betty Maina na Eric Wamumbi wafunga ndoa

0
kra

Wabunge Betty Maina anayewakilisha kaunti ya Murang’a na Eric Wamumbi wa eneo bunge la Mathira walifunga ndoa ya kitamaduni Jumamosi Novemba 18 huko Murang’a.

Harusi hiyo ilihudhuriwa na viongozi wengi wa upande wa upinzani na wale wa upande wa serikali wakiongozwa na naibu rais Rigathi Gachagua.

kra

Wabunge wengi wa kike walivaa mavazi ya kufanana na walimsindikiza Bi harusi huku wa kiume nao ambao walivalia mavazi sawia wakimsindikiza Bwana harusi.

Picha zilizosambaa mitandaoni zilionyesha viongozi kadhaa wakicheza densi za utamaduni wa jamii ya Agikuyu.

Wabunge wa upande wa upinzani waliokuwepo ni pamoja na mbunge wa Lang’ata Phelix Odiwuor almaarufu Jalang’o, mbunge mteule wa chama cha ODM Irene Mayaka, mbunge wa Suba Kaskazini Millie Odhiambo na Peter Salasya wa Mumias Mashariki kati ya wengine.

Mheshimiwa Millie Odhiambo alisifia harusi ya wabunge hao wawili akisema, “Harusi ya waheshimiwa Betty na Eric katika kaunti ya Muranga ilifana sana na ni ya aina yake. Sijawahi kuona wabunge wawili wakifunga ndoa labda hawandio wa kwanza katika historia ya nchi hii. Mungu abariki ndoa yenu.

Mbunge mteule Irene Mayaka naye alipongeza wawili hao, akawatakia kila la heri katika maisha yao ya ndoa huku akisifia hafla hiyo ambayo alisema ilikuwa ya kufana.

Website | + posts